Umoja wa Ulaya Yaliyomo Historia | Wakazi | Uhuru wa kuhama | Vyombo vya Umoja | Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya | Viungo vya Nje | Urambazajiwww.europa.euEuropean UnionEuropean Union online portalFinland's EU Council Presidency'Your Europe' information websiteEuropedia: Guide to European policies and legislationkuihariri na kuongeza habari
Mbegu za jiografia ya UlayaSiasaUmoja wa UlayaMashirika ya kimataifaBrussels
kifupishoUlaya1991Jumuiya ya Kiuchumi ya UlayauchumivitapesaEuroJumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya1992mikataba ya MaastrichtsiasaMapatano ya Schengenpasipoti20042007Kroatia2103Quai d'OrsayBrusselsFrankfurtDonald TuskCecilia Malmströmmilioni2013LondonParislughalugha rasmiKiingerezaKijerumaniKiitaliaKifaransadiniWakristoWakatolikiWaprotestantiWaorthodoksiWaislamuWakanamunguuraiakazibiasharabidhaa
Umoja wa Ulaya
Jump to navigation
Jump to search
www.europa.eu |
Umoja wa Ulaya (kifupisho: EU) ni muungano wa kisiasa na wa kiuchumi wa nchi 28 za Ulaya.
Ulianzishwa mwaka 1991 juu ya msingi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya.
Shabaha kuu zilikuwa kujenga uchumi wa pamoja, kuboresha maisha ya watu wa Ulaya na kuzuia vita kati ya nchi za Ulaya.
Nchi 18 za Umoja huo hutumia pesa moja ya Euro.
Nchi nyingi za Umoja zimepatana kufungua mipaka yao bila vizuizi kwa wakazi wote.
Yaliyomo
1 Historia
2 Wakazi
3 Uhuru wa kuhama
4 Vyombo vya Umoja
4.1 Halmashauri ya Ulaya
4.2 Baraza za mawaziri
4.3 Kamati ya Ulaya
4.4 Bunge la Ulaya
5 Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya
5.1 Wanachama tangu 1958 (waanzilishaji)
5.2 Wanachama tangu 1973
5.3 Mwanachama tangu 1981
5.4 Wanachama tangu 1986
5.5 Wanachama tangu 1995
5.6 Wanachama tangu 2004
5.7 Wanachama tangu 2007
5.8 Wanachama tangu 2013
5.9 Nchi zinazoomba uanachama
6 Viungo vya Nje
Historia |
Jumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya ilibadilisha jina lake mwaka 1992 kufuatana na mikataba ya Maastricht kuwa Umoja wa Ulaya.
Nchi wanachama zilipatana kujenga siasa ya pamoja ya kiuchumi, kifedha, kisheria na katika mambo ya nje.
Mapatano ya Schengen ilifungua mipaka ili wakazi wa nchi hizo waweze kusafiri bila pasipoti wala vibali.
Nchi 10 tena zilijiunga na Umoja wa Ulaya mwaka 2004. Mbili zaidi ziliingia 2007 na Kroatia mwaka 2103.
Quai d'Orsay (Brussels)
Euro Tower (Frankfurt)
Donald Tusk (2017)
Cecilia Malmström
Wakazi |
Jumla ya wakazi ni milioni 507.4 (2013). Kuna miji 16 yenye watu zaidi ya milioni moja kila mmojawapo, kuanzia London na Paris ambayo inazidi milioni 10.
Upande wa lugha, lugha rasmi ni 24, lakini lugha inayotumika zaidi ni Kiingereza, kinachoweza kuzungumzwa na 51% za wakazi wote, ingawa ni lugha ya kwanza ya 13% tu. Lugha nyingine ambazo ni za kwanza kwa wananchi wengi ni: Kijerumani (16%), Kiitalia (13%) na Kifaransa (12%). Pia kuna lugha 150 hivi za kieneo.
Upande wa dini, wakazi wengi ni Wakristo (72%), hasa Wakatoliki (48%), Waprotestanti 12% na Waorthodoksi 8%. Waislamu ni 2%. Wengine hawana dini au ni Wakanamungu.
Uhuru wa kuhama |
Kila mtu mwenye uraia wa nchi ya Umoja anaruhusiwa kuhamia nchi yoyote nyingine na kufanya kazi au biashara huko bila vibali vya pekee.
Vilevile bidhaa zote zinazotengenezwa kote katika Umoja wa Ulaya zinaweza kuuzwa katika kila nchi. Hii ni sababu ya kuwa na sheria za pamoja zinazotawala masharti ya bidhaa na uzalishaji.
Vyombo vya Umoja |
Halmashauri ya Ulaya |
Halmashauri hii ni mkutano wa viongozi wa serikali za nchi wanachama. Wanakutana mara mbili kwa mwaka na kutoa maazimo muhimu.
Nafasi ya uraisi hubadilika kila baada ya miezi 6. Ufini ilishika uraisi kati ya Julai 2006 hadi Desemba 2006, ikafuatiliwa na Ujerumani tangu Januari hadi Juni 2007.
Baraza za mawaziri |
Katika baraza hizi mawaziri ya Kilimo, Sheria, Mambo ya Nje hukutana na kupanga siasa ya pamoja.
Kamati ya Ulaya |
Hii ni kamati ya utawala inayotekeleza maazimio ya Halmashauri na bunge. Kuna makamishna 24 na mwenyekiti. Inaelekea kuwa serikali lakini haina madaraka ya serikali bado.
Bunge la Ulaya |
Bunge la Ulaya lina wabunge 751 wanaochaguliwa na wananchi kila baada ya miaka mitano.
Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya |
Wanachama tangu 1958 (waanzilishaji) |
- Ubelgiji
- Ufaransa
Ujerumani*- Italia
- Luxemburg
- Uholanzi
Wanachama tangu 1973 |
- Denmark
- Ueire
- Uingereza
Mwanachama tangu 1981 |
- Ugiriki
Wanachama tangu 1986 |
- Ureno
- Hispania
Wanachama tangu 1995 |
- Austria
- Ufini
- Uswidi
Wanachama tangu 2004 |
- Kupro
- Ucheki
- Estonia
- Hungaria
- Latvia
- Lithuania
- Malta
- Poland
- Slovakia
- Slovenia
Wanachama tangu 2007 |
- Bulgaria
- Romania
Wanachama tangu 2013 |
- Kroatia
Nchi zinazoomba uanachama |
- Masedonia
- Serbia
- Uturuki
Viungo vya Nje |
- European Union online portal
- Finland's EU Council Presidency
- 'Your Europe' information website
- Europedia: Guide to European policies and legislation
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Umoja wa Ulaya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Jamii:
- Mbegu za jiografia ya Ulaya
- Siasa
- Umoja wa Ulaya
- Mashirika ya kimataifa
- Brussels
(RLQ=window.RLQ||[]).push(function()mw.config.set("wgPageParseReport":"limitreport":"cputime":"0.088","walltime":"0.115","ppvisitednodes":"value":291,"limit":1000000,"ppgeneratednodes":"value":0,"limit":1500000,"postexpandincludesize":"value":2446,"limit":2097152,"templateargumentsize":"value":63,"limit":2097152,"expansiondepth":"value":9,"limit":40,"expensivefunctioncount":"value":1,"limit":500,"unstrip-depth":"value":0,"limit":20,"unstrip-size":"value":3351,"limit":5000000,"entityaccesscount":"value":0,"limit":400,"timingprofile":["100.00% 17.898 1 -total"," 72.83% 13.035 1 Kigezo:Lango"," 56.96% 10.195 1 Kigezo:Portal_box"," 27.73% 4.963 1 Kigezo:Portal/core"," 13.83% 2.475 1 Kigezo:Commons"," 12.39% 2.217 1 Kigezo:Mbegu-jio-Ulaya"," 10.38% 1.858 1 Kigezo:Portal/Images/Ulaya"],"cachereport":"origin":"mw1303","timestamp":"20190521224838","ttl":2592000,"transientcontent":false););"@context":"https://schema.org","@type":"Article","name":"Umoja wa Ulaya","url":"https://sw.wikipedia.org/wiki/Umoja_wa_Ulaya","sameAs":"http://www.wikidata.org/entity/Q458","mainEntity":"http://www.wikidata.org/entity/Q458","author":"@type":"Organization","name":"Uchangiaji katika miradi ya Wikimedia","publisher":"@type":"Organization","name":"Wikimedia Foundation, Inc.","logo":"@type":"ImageObject","url":"https://www.wikimedia.org/static/images/wmf-hor-googpub.png","datePublished":"2006-12-29T15:06:25Z","dateModified":"2018-11-30T13:15:48Z","image":"https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/b/b7/Flag_of_Europe.svg"(RLQ=window.RLQ||[]).push(function()mw.config.set("wgBackendResponseTime":216,"wgHostname":"mw1242"););